DODOMA YETU

DODOMA NI MJI MKUU WA TANZANIA.

FAHAMU MAMBO NA MAENEO MENGI KATIKA MKOA HUU WA DODOMA KUPITIA CAPITAL CITY TZ BLOG .

Mkoa wa Dodoma

Mahali pa Mkoa wa Dodoma katika Tanzania
Mkoa wa Dodoma
Mkoa wa Dodoma uko katikati ya Tanzania umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida. Sehemu kubwa ya eneo lake ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB.
Eneo lote la mkoa lina 41,310 km². Kuna wilaya saba zifuatazo:
Wilaya ya Bahi, Wilaya ya Chamwino, Wilaya ya Chemba, Wilaya ya Dodoma Mjini, Wilaya ya Kondoa, Wilaya ya Kongwa, Wilaya ya Mpwapwa. Wilaya ya awali ya Dodoma Vijijini imegawiwa kwa wilaya mpya za Chamwino na Bahi.
Katika sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Mkoa wa Dodoma ilihesabiwa kuwa 2,083,588. [1]
Mnamo Machi 2012 ilianzishwa wilaya mpya ya Chemba.

Mawasiliano

Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia mji wa Dodoma kwenda Morogoro - Daressalaam, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.

Hali ya hewa na kilimo

Kwa jumla Dodoma haina mvua nyingi isipokuwa sehemu za wilaya za Mpwapwa na Kondoa. Hivyo hasa mazao yasiyotegemea sana mvua hulimwa kama vile mtama, wimbi, muhogo; kilimo cha mahindi hupatikana mara kwa mara na matatizo ya kukosa mvua. Mazao ya sokoni ni karanga alizeti na simsim. Dodoma ni pia mwanzo wa ustawishaji wa mizabibu na uzalishaji wa divai katika Tanzania.
Kutokana na hali ya hewa mifugo ni mingi (ng'ombe 1,600,000, mbuzi 954,000, kondoo 274,000, nguruwe 23,000, kuku takriban 1,400,000). Idadi ya mifugo imeongeza tatizo la mmomonyoko wa ardhi katika sehemu za Mkoa wa Dodoma.

Wakazi na utamaduni

Idadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo. Kondoa kuna Wangulu na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Wanasemekana ya kwamba babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini. Kongwa kuna Wakaguru, Wagogo, na Wamasai; na Mpwapwa kuna Wahehe, Wagogo, na Wakaguru.

ya muungano wa Tanzania.Na pia umebahatika kuwa na Ikulu ndogo iliyopo Chamwino katika wilaya ya Chamwino.Mkoa wa DODOMA ni maarufu kwa kilimo cha karanga na Zabibu.Mkoa huu umepata bahati ya kuwa na vyuo vingi sana ambavyo vimesaidia kupunguza tatizo la ajira .UDOM ni moja ya vyuo vikubwa sana nchini Tanzania ambacho kinatowa wahitimu waliokwiva kwenye idara husika.

PICHA ZA CHUO KIKUU CHA UDOM





PICHA ZIFUATAZO NI ZA MAENEO TOFAUTI TOFAUTI YA MKOANI DODOMA