WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliyeondolewa ofisini hivi karibuni kutokana na sakata la Tegeta Escrow, Anna Tibaijuka, hivi karibuni amenaswa akiwatembelea watu wanaosadikiwa kuwa wapiga kura wake jimboni Muleba mkoani Bukoba akiwa pekupeku.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof.Anna Tibaijuka akipekua jimboni Muleba mkoani Bukoba.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, vikiwemo mitandao ya kijamii, Waziri
huyo Profesa, ameamua kuwafuata wapiga kura wake popote walipo jimboni
kwake, kwa ajili ya kujiweka sawa wakati huu nchi ikijiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, Oktoba mwaka huu.
Prof.Anna Tibaijuka akiwa na watu wanaodaiwa kuwa ni wapiga kura wakejimboni hapo.
“Lile sakata la Escrow limemchanganya sana Profesa, anaamini maadui
zake kisiasa wanalitumia kama fimbo ya kumchapa, anachofanya ni
kuwapitia wapiga kura wake na kuwaeleza ukweli na kwa kadiri anavyozidi
kuwafikia, wengi wanaonekana kumwelewa,” alisema mtu mmoja anayefuatilia
safari za Waziri Tibaijuka, ambaye ni mmiliki wa kampuni ya VIP,
inayodaiwa kuuza hisa zake za IPTL, James Rugemalila, alimuingizia kiasi
cha shilingi bilioni 1.6 kwenye akaunti yake binafsi, fedha ambazo
baadaye, mtumishi huyo wa umma alidai zilitolewa kwa nia njema, kwa
ajili ya kuwasaidia kimasomo wasichana.
Prof.Anna Tibaijuka wakati akiwa Bungeni.
Katika picha zinazoonekana katika mitandao, Profesa Tibaijuka, ambaye
aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Makazi wa Umoja wa Mataifa (INHABITAT),
anaonekana akiwa na baadhi ya akina mama walitembelea kaya mbalimbali
jimboni mwake. Aidha moja ya picha hizo, zinamuonyesha akiwa na familia
moja nje ya kibanda chao cha bati.Amani lilimtafuta Profesa Tibaijuka ili kuzungumzia suala hilo, lakini alipopatikana, aliomba kupigiwa baadaye kwani kwa wakati huo,alidai kuwepo kikaoni. Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, simu ya kiongozi huyo ilikuwa ikiita bila kupokelewa.