Thursday, June 4, 2015

WAZAZI WAMTAKA WOLPER AKAISHI NYUMBANI KWAO

Waandishi wetu
MTU kwao! Licha ya kuwa staa wa muvi za Bongo, mwigizaji kiwango, Jacqueline Wolper Massawe anadaiwa kuitwa na wazazi wake kwenda kuishi nyumbani kwao, Kibaha mkoani Pwani ili kuepukana na
skendo za kila mara za mjini.
Staa wa muvi za Bongo, mwigizaji kiwango, Jacqueline Wolper Massawe.
Kwa mujibu wa chanzo, Wolper amewekewa msimamo huo na wazazi wake, hususan mama yake mzazi aliyemwambia kwa kuwa ana usafiri anaweza kuishi huko na kufika jijini Dar kwa kazi za mchana kutwa kisha kurudi Kihaba kwa malazi na makazi.
Wolper alipotafutwa kuulizwa kuhusu hilo, alijibu: “Kweli wazazi wangu wanapenda niwe nao karibu wakiamini nitaendelea kuwa mtoto mzuri bila skendo, lakini inakuwa ngumu ndiyo maana utakuta mara nyingi niko kule lakini kimakazi niko Dar, nitafikiria.”