Friday, July 10, 2015

SIKU YA PSPF YAFANA SABASABA

Wasanii Mrisho Mpoto na Kundi la Orijino Commedi.


Mpoki wa Orijino Komedi. Wananchi wakijiunga na PSPF.
WENGI WAJIUNGA NA MFUKO
ORIGINAL KOMEDI WAWA KIVUTIO
Na Mwandishi Wetu
Siku ya PSPF iliyoandaliwa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF ilifana na kuvutia mamia ya wananchi waliotembelea maonesho ya 39 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yaliyomalizika hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Siku hiyo ni maalum kwa ajili ya kutoa elimu ya Mfuko wa PSPF kwa umma ili waweze kupata uelewa mpana wa sekta ya Hifadhi ya Jamii hususan bidhaa na huduma zinazotolewa na PSPF. Kwa mwaka huu, PSPF ililenga kuhimiza watanzania kujiunga na Hifadhi ya Jamii kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari unaoendeshwa na PSPF.
Kwa mujibu wa takwimu zilizipo zaidi ya asilimia 90 ya Watanzania hawapo katika Hifadhi ya Jamii, hivyo jukumu kubwa la siku ya PSPF mwaka huu ni kuhakikisha watanzania wengi wanajiunga na PSPF, jambo hilo lilifanikiwa kwani zaidi ya watu 500 walijiunga na PSPF katika maonesho ya sabasaba ya mwaka huu.
Siku hiyo ilitumika kuwa hamasisha wanachama wa PSPF kuwa na utaratibu wa kuhakiki taarifa zao mbalimbali ikiwemo, historia ya michango, historia ya pensheni, kufuatilia mafao, kujisajili katika Mfuko na pia PSPF ilikuwa ikitoa vitambulisho vipya kwa wanachama wake.
Katika kunogesha siku ya PSPF, Mfuko uliwaalika, Balozi wa PSPF Mjomba Mrisho Mpoto, waigizaji wote wa kikundi cha Original Komedi na Mboni Masimba mtangazaji na mwaandaaji wakipindi cha The Mboni Show kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha TBC, kwa udhamini wa PSPF
Baadhi ya wageni mashuhuri waliotembelea banda la PSPF wakati wa maonesho hayo ni pamoja na Mheshimi wa Jakaya Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Gaudensia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira, Mheshimiwa Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Shaaban Lila, Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania na wengine wengi.
Kwa mwaka wa pili mfululizo Mfuko wa Pensheni wa PSPF umekuwa ukitenga siku maalum wakati wa maonesho ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (sabasaba) kwa ajili ya kutoa elimu juu ya Sekta ya Hifadhi ya Jamii na huduma zinazotolewa na PSPF.