Friday, July 10, 2015

TMK WANAUME HALISI KUJA NA TAMASHA LA MUZIKI IDD PILI


Muongozaji wa tamasha hilo, Ally Coco (kushoto) akizungumza na wanahabari (hawapo pichani)pamoja na Rich One.
Wanahabari wakichukua tukio.
Wakisikiliza kwa makini.
UONGOZI wa Kundi la Muziki la TMK Wanaume Halisi lenye maskani yao, Temeke jijini Dar umeandaa tamasha kubwa la muziki siku ya Idd Pili, mwaka huu lenye lengo la kuadhimisha miaka 30 ya Shule ya Sekondari ya Jitegemee.

Akizungumza na wanahabari leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (Maelezo), kiongozi wa tamasha hilo, Ally Coco amesema kuwa Tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya TTC Chang’ombe jijini Dar es Salaam na lengo kubwa ni kuandhimisha miaka 30 ya Shule ya Jitegemee na kutoa tuzo kwa wasanii ambao vipaji vingi vyao vimetoka shule hiyo.
Alisema kuwa baadhi ya wasanii ambao watapewa tuzo hiyo ni Ray Kigosi, Masogange, Kajala, Seven, Rich One, Soggy Doggy, Mhe.Temba, Kisoki, Chid Benz, pamoja na Ras Pompidoo kutoka In Afrika Band ambao wote vipaji vyao vilitokana na kusoma shule hiyo ya Jitegemee ya Jeshi.
Mbali na wasanii hao pia aliwataja baadhi ya wachezaji wa mpira maarufu hapa nchini waliosoma shule hiyo kama, Credo Mwaipopo, Renatus Njohore, Waziri Mahazi, Ally Mayai, pamoja na Mwandishi wa Habari, Edo Kumwembe.
Aidha amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na burudani ya  wasanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka kwa Pam D, Juma Nature, Soggy Doggy, Msaga Sumu, Matonya, Mapacha Watatu, Mr.Blue pamoja na Jay Moe.
Hata hivyo amesema kuwa siku hiyo kutakuwa na nyama choma kwa wapenzi na kiingilio kitakuwa shingi 5,000/= kwa watakao wahi kuchukua tiketi siku moja kabla na shilingi 7,000/= mlangoni ambapo tiketi zitapatikana shule ya Jitegemee na Viwanja vya TCC Chang’ombe ambapo kiasi kitakachopatikana siku hiyo kitatumika katika ujenzi unaoendelea wa ukumbi mpya wa mikutano katika shule hiyo.