Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili
kushoto) akiongoza kikao cha Kamati Kuu Maalum cha CCM mjini
Dodoma,
Kikao kilichochuja majina ya wagombea na kupata majina matano.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman
Kinana akitoa taarifa fupi ya wajumbe waliohudhuria kikao cha Kamati Kuu
Maalum ambapo wajumbe 28 walihudhuria kati ya 32.
Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakipitia baadhi ya makabrasha wakati wa kikao cha Kamati Kuu Maalum.
Vijana wa CCM wakipakia mikoba
yenye makabrasha ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa 2015 ambao
umeshaanza hivi punde katika ukumbi mpya wa Dodoma Convention Centre
mjini Dodoma uliozinduliwa juzi.