Mwalimu wa Shule ya Sekondari Manushi Kibosho, Wilaya ya Moshi Vijijini ameuawa saa chache baada ya ugomvi unaohusishwa na kuchanwa kwa picha ya mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Mwalimu
huyo, Demetus Dastan (33) maarufu kwa jina la Kidule, aliuawa Jumamosi
iliyopita usiku na mwili wake kukutwa katika shamba la mtu aliyetajwa
kuwa ni Joackim Massawe.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Fulgence Ngonyani alisema kabla ya
kuuawa, mwalimu huyo alikuwa amekwenda kunywa pombe katika klabu moja
hapo kijijini. Inadaiwa kuwa akiwa klabuni, kulitokea ubishani kati yake
na mtu mwingine uliotokana na kuchanwa kwa picha ya Lowassa ambao
ulikwenda mbali na kusababisha wapigane.
Kamanda
Ngonyani alisema waliamuliwa na wateja wengine waliokuwapo na baadaye
mwalimu huyo aliondoka kurejea nyumbani na hakuonekana hadi mwili wake
ulipookotwa.
Baadaye
mwili wake ulikutwa shambani ukiwa na michubuko kidogo kwenye mguu wa
kulia karibu na goti na shati lake likiwa limechanikachanika.
Polisi
wamewakamata watu wawili akiwamo mmiliki wa klabu hiyo na mtu mwingine
anayedaiwa kuwa aliongozana naye kurudi nyumbani huku mtu waliyepigana
naye akiendelea kusakwa.