MATUKIO KATIKA PICHA KUTOKA BUNGENI DODOMA
Baadhi ya Maofisa
Habari Mawasiliano wa Wizara za Serikali, wakielekea katika Ukumbi wa Mkutano wa Bunge mjini Dodoma, leo. Maafisa hao wamefanya ziara Bungeni hapo ili kuona shughuli za Bunge.
Baadhi ya
Maafisa Habari Mawasiliano Serikalini wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Assah Mwambene (wa nne kutoka kushoto mstari wa mbele). Wakiwa
ndani ya ukumbi wa Bunge leo kuangalia shughuli za Bunge mjini Dodoma.
Baadhi ya Maafisa
Habari Mawasiliano Serikalini wakiwa ndani ya ukumbi wa Bunge.
Naibu Waziri, Ofisi
ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) Aggrey Mwanri
akiwakilisha hati mezani kuhusu Taarifa ya
Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa na Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa
kwa Mwaka wa Fedha,2010/2011.
Naibu Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi Pereira Silima akiwasilisha azimio la Bunge la Kujiunga na
Mkataba wa Kimataifa wa Kuzuia Vitendo vya Ugaidi wa Kutumia Nyuklia. Azimio
hilo limeungwa mkono leo katika mkutano wa kumi kikao cha nane.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Shukuru Kawambwa
(kulia) akiongea na James Mbatia
(Kushoto)- katika viwanja vya Bunge leo. Baada ya Spika Anne Makinda(hayupo pichani) kutangaza
rasmi Mitala ya Elimu inayotumika ni
halali na ipo. (Pichani katikati) ni
Charles Mwijage (Muleba Kaskazini).
Mwenyekiti wa Bunge
Mussa Zungu Azzan akifafanua kanuni mbalimbali
Bungeni leo.
Kiongozi wa
Kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe(kushoto) akiongea na Joshua Nassari(Arumeru Mashariki) ndani ya ukumbi
wa Bunge. Picha Mwanakombo
Jumaa- MAELEZO.
No comments:
Post a Comment