Takriban watu 27 wakiwemo watoto na wanawake wameuawa katika mapigano Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Yanaaminika kuwa mapigano ya kikabila. Waathiriwa wote walikuwa watu wa kabila la Bafuliru.
Haijulikani nani aliyetekeleza mashambulizi hayo lakini eneo hilo limeshuhudia mgogoro kati ya watu wa kabila la Bafuliru na Barundi
Mwandishi wa shirika la habari la Reuters alisema kuwa waathiriwa walipigwa risasi , kudungwa visu au kuchomwa wakiwa ndani ya nyumba zao.
Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la Kivu Kusini, Jean-Julien Miruho aliambia shirika la habari la Agence France Presse kuwa uvamizi huo ulikuwa uvamizi wa kulipiza kisasi kwa wizi wa mifugo.