Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, mmoja wa marafiki zake wa karibu ambaye aliomba chondechonde asitajwe gazetini alisema kwamba, mara ya mwisho kuona chozi la Wema ni siku ya msiba wa marehemu baba yake, mzee Isaac Sepetu lakini hili lilizidi kilio kile kwani ni tukio la udhalilishaji kwa mzazi wake huyo hivyo kuzimia ilikuwa ni lazima kwani yaliyomkuta yanasikitisha.
Chanzo hicho kilidai kwamba, Wema hakutegemea kama ipo siku mama yake atadhalilishwa kiasi hicho hadi kufikia yeye kupoteza fahamu.
“Kiukweli ile picha ilichafua sana hali ya hewa hasa kwa wanaompenda Wema na hata kwa wanaomchukia Wema kwani kila mmoja alikuwa analaani kitendo kile ambacho si cha kiungwana.
“Unajua inafika hatua unatakiwa ufahamu mama wa mwenzio ni mama yako pia halafu usifurahie ubaya anaofanyiwa mama wa mwenzio tutukanane sisi wenyewe na si kuwaingiza wazazi kwenye mambo wasiyojua mbele wala nyuma,” kilidai chanzo hicho.
“Hebu fikiria mama yako mzazi atengenezewe picha ya utupu na jamii iaminishwe kuwa ni yeye wakati si kweli, inauma sana jamani. Utadhani huyo mtu hajazaliwa na mama
.”
TIMU DENGUE NA MKAKATI MZITO
Katika kipindi cha vuguvugu la kuchafuana kilichoanza mwanzoni mwa wiki iliyopita, kuna wachangiaji katika mitandao ya kijamii waliojiita kwa jina la Timu Dengue, walionekana kumkandia Wema.
Chanzo chetu kinadai kuwa, timu hiyo ina mkakati mzito wa kumchafua Wema kwa kila namna.
“Wamepanga mkakati mzito, wanadai eti Wema anajisikia. Lakini watu wanasema haiwezekani watu wafanye mambo bila sababu. Sasa hapo wanamhusisha Kajala (Masanja) kwa kuwa ndiye mtu aliye na bifu naye kwa sasa,” kilipasha chanzo hicho na kuongeza:
“Lakini kuna wengine wanabishana, wanadai kuwa inawezekana watu wasio na kazi za kufanya au wenye chuki binafsi na Wema wameamua kutumia mwanya huo kumchafua Wema na familia yake wakiamini lazima Kajala atahusishwa kwa kuwa ana ugomvi naye.”
BOFYA HAPA KUMSIKIA WEMA
Risasi Mchanganyiko iliposhuhudia picha hiyo ya utupu na kujiridhisha kuwa siyo ya mama Wema, lilimtafuta Wema kuzungumzia ni kwa jinsi gani alivyoumia baada ya kuona picha ile ambapo majibu yake alionekana bado ana maumivu makali ambayo yalidhihirisha wazi yalikuwa hayajamuisha moyoni.
“Nimeumia sana mama yangu kudhalilishwa na si mimi tu familia yangu yote kwa jumla, tumeumizwa sana kwa tukio lile lakini mimi nasema namuachia Mungu kwani yeye ndiye anajua ila siyo siri ni tukio ambalo lilinifanya niugue ghafla,” alisema Wema na kuongeza:
“Yaani nilikuwa napewa pole nyingi sana utadhani mimi mgonjwa. Hata wale ambao hawanipendi nao walikuwa wakinipa pole. Naomba serikali itazame upya hili suala hili la watu kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii.”
AUNT EZEKIEL AFANYA KAZI YA ZIADA
Katika ishu hiyo, staa mwenzake wa sinema za Kibongo ambaye kwa sasa ni mashosti, Aunt Ezekiel Grayson alifanya kazi ya ziada kumuokoa Wema na kumfariji asichukue uamuzi mgumu.
Inaelezwa kuwa, Aunt alitumia dakika 29 kumpepea shosti wake huyo ili aweze kurejewa na fahamu, jambo zoezi ambalo lilizaa matunda.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko, Aunt alisema tukio hilo limemuumiza kila mtu hata wale ambao wanaonekana wako tofauti na Wema lakini kwa hili nao wameumia na kuungana naye kumtetea na kuwakemea waliyofanya kitendo kile.
“Nimeumia kwa tukio ambalo limefanywa na kusababisha Wema wangu kulia sana hadi kufikia kuumwa ghafla na kupoteza fahamu. Dah! Binadamu wengine sijui tukoje, lakini hamtaweza kufanikisha kwa sababu Wema ana watu wengi wanaompenda kuliko wanaomchukia,” alisema Aunt.
KAJALA SASA
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Kajala kupitia simu yake ya mkononi ili kujibu tuhuma za kuhusishwa na picha hiyo lakini simu yake ilikuwa ikikatika kila ilipopigwa.
Baadaye ilijulikana kuwa, aliamua kuifunga kwa muda (inawezekana alikuwa sehemu inayohitaji utulivu).
Baadaye akatumiwa ujumbe uliosomeka: “Habari. Una taarifa ya picha chafu ya kutengenezwa ya mama Wema iliyosambazwa mitandaoni? Lakini unatajwa kuhusika kwa sababu una bifu na Wema, unasemaje?”
Hata hivyo, tunakwenda mitamboni, Kajala hakujibu meseji hiyo wala kupiga simu chumba cha habari kufafanua kuhusiana na madai hayo ambayo bado hayajathibitishwa.
MAMA WEMA ANASEMAJE?
Jitihada za kuzungumza na mama Wema juu ya sakata hilo ziligonga mwamba kwani simu yake iliita bila kupokelewa.
SERIKALI NAYO
Timu yetu ilijaribu kufanya mawasiliano na Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Mhe. January Makamba bila mafanikio, kwani simu yake haikupatikana.
Hata hivyo, wananchi wametoa kilio chao kwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kudhibiti usambazwaji wa picha chafu mitandaoni.
TUJIKUMBUSHE
Hivi karibuni, kuliibuka picha chafu katika mitandao ya kijamii za waheshimiwa wabunge, kabla ya baadaye wabunge kulaan ambazo mpaka sasa hazijulikana kuwa zilikuwa halisi au za kutengen
TAHADHARI
Kumekuwa na wingu la kuchafuana kwenye mitandao ya kijamii ambapo ukiacha watu maarufu kutengenezewa picha chafu pia wanafunzi wa vyuo wamekuwa waathirika wakubwa hivyo ni vyema kila mtu akachukua taadhari na mamlaka husika ilishughulikie.
No comments:
Post a Comment