INASIKITISHA! Mzee aliyejulikana kwa jina la Oscar, mkazi wa Kiwalani jijini Dar, anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la kudaiwa kusababisha kifo cha mtoto Suzan Justin mwenye umri wa miezi tisa.
Kwa mujibu wa mama mzazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Veriana Peter, kwenye tukio hilo lililotokea hivi karibuni, mwanaye alikuwa akisumbuliwa na mafua, akamuacha sebuleni na kwenda kujiaandaa chumbani ili ampeleka hospitali.
Akiwa chumbani, ghafla alisikia mtoto akilia kwa sauti na alipotoka alimkuta mwanaye akiwa chini karibu na friji huku akilia sana. “Sikujua nini kimetokea, nikamchukua na kwenda naye hospitali ya Amana.
“Baada ya kufika hospitalini hapo huku mtoto akiendelea kulia manesi walimpima na kuniambia kama
mtoto alianguka basi ni kawaida kulia, wakanipa dawa za kutuliza maumivu nikarudi nyumbani.
“Tulivyofika nyumbani mtoto hakulala siku hiyo, aliendelea kulia, kesho yake nikamrudisha tena Amana. Nikaambiwa niende Muhimbili (Hospitali ya Taifa) kwani wao wameshindwa kutambua tatizo la mwanangu.
“Nikaenda Muhimbili, mtoto alipoangaliwa na kuchukuliwa vipimo madaktari wakaniambia nimechelewa kwani damu ilikuwa imevilia kichwani na baada ya siku moja mtoto alifariki,” alisema mzazi huyo.
Baada ya mtoto kufariki, mama huyo alirudi
nyumbani ili kuendelea na taratibu za mazishi, ndipo mdogo wake alitoa
madai kuwa alimuona babu yake akimuweka mtoto huyo juu ya friji kisha
akaanguka.
...Kiongozi wa dini akiongoza mazishi ya SuzanBaadhi ya waombolezaji waliposikia maneno hayo, walianza kupiga kelele za kutaka kuandamana huku vurugu zikizidi, polisi walitonywa na wasamaria wema na wakafika eneo hilo na kumkamata Oscar, wakampeleka kituo cha polisi cha Buguruni kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Kwa upande wake baba mzazi wa mtoto huyo, Justin Bernad alisema:
“Kifo cha mwanangu kinaniumiza sana ni ngumu kuamini kutokana na mazingira yenyewe lakini namuachia Mungu, najua ana makusudi na mimi lakini hata sheria itafuata mkondo na ukweli utajulikana.”
Marehemu Suzan Justin enzi za uhai wake.
Oscar amefunguliwa majalada mawili yaliyosomeka hivi;
BUG/RB/1235/2014, KIFO CHA MASHAKA na BUG/RB/12291/2014, SHAMBULIO LA
KUDHURU MWILI.