Wednesday, July 9, 2014

Kuhusu kiwanda cha Samsung kuvamiwa na wezi Brazil katika mji wa Sao Paulo.


samsung-brazil
Inadaiwa kuwa Wezi wamevamia kiwanda cha simu cha Samsung nchini Brazil usiku na kuiba mali yenye thamani ya dola milioni 36.
Mali hiyo ilikuwa pamoja na simu za mkononi na kompyuta.

samss
Genge hilo lililokuwa limejihami vikali, liliwateka wafanyakazi wanane waliokuwa wanaodnoka kazini na kuiba vitambulisho vyao ambavyo walivitumia kuweza kuingia katika kiwanda hicho mjini Sao Paulo.
Inaarifiwa wezi hao waliwazidi nguvu walinzi na kuchukua muda wa saa tatu kufanya wizi huo.
Polisi wanasema kuwa genge hilo lilikuwa na wezi, 20 ambao walifanikiwa kuiba simu 40, 000 pamoja na tarakilishi, tabiti na vifaa ningine vyenye thamani ya dola milioni 36.

No comments:

Post a Comment