Rais Obama anaomba dola bilioni
3.7 za msaada wa dharura kutoka bunge la Marekani kusaidia kukabiliana
na ongezeko la watoto waliohama peke yao kutoka Amerika ya kati.
Ikulu ya Marekani inasema fedha hizo zitasaidia
kupunguza kile maafisa wanakitaja kuwa hali ya dharura ya kibinaadamu
iliyoshuhudia watoto zaidi ya elfu hamsini na mbili waliohama peke yao
kutoka El Salvador, Guatemala na Honduras kuvuka kiharamu mpaka wa
Marekani tangu mwezi Oktoba mwaka jana.Wengi wao watoto ambao wameingia Marekani kupitia bonde la Rio Grande huko Texas.
Rais Obama ameielezea hali kuwa mzozo wa kibinaadamu na sasa anaomba mabilioni ya dola kutoka bunge nchini humo kuharakisha kushughulikiwa na kusafirishwa kwa wahamiaji hao, vile vile kuongeza ukaguzi na kuyasaka makundi ya kihalifu yanayosaidia kusafirishwa kiharamu kwa wahamiaji katika mpaka.
Kampeni katika vyombo vya habari katika nchi wanazotoka wahamiaji hao, inatarajiwa pia kuondosha fikra kwamba watoto wanaowasili Marekani kiharamu wataruhusiwa kukaa.
Licha ya makubaliano kwamba mfumo huo unahitaji mageuzi ya dharura, bunge limetatizwa na iwapo wabadilishe mfumo mzima wa uhamiaji nchini.
No comments:
Post a Comment