Tuesday, December 2, 2014

Aliyewakosoa Sasha na Malia ajiuzulu



Sasha na Malia walikosolewa kwa kuvalia sketi fupi mbele ya umati katika White House
Mfanyakazi katika chama cha Republican nchini Marekani amejiuzulu baada ya kukosolewa kwa kuwatuhumu wanawe Rais wa Marekani Barack Obama , Sasha na Malia kwa kuwaambia kuwa wamekosa ustaarabu.
Elizabeth Lauten, afisaa mkuu wa mawasiliano wa mwanasiasa mkuu wa chama hicho, Stephen Fincher, alijiuzulu Jumatatu.
Bi Lauten, aliwakosoa watoto wa Obama Sasha na Malia kwenye ukurasa wake wa Facebook baada ya watoto hao kuonekana wakiwa wamevalia sketi fupi kwenye hafla ya jioni.
Rais Obama na mkewe wamejitahidi sana kuwalinda watoto wao kutokana na ndimi kali za vyombo vya habari
Baadaye Lauten alifuta maandiko yake ambayo baadaye aliyataja ya kuumiza moyo na kuudhi.

Bi Lauten pia alikuwa amewakosoa Sasha na Malia kwa kusema walionekana wasio na furaha walipokuwa wamesimama na baba yao katika hafla ya maankuli katika Ikulu ya White House.
Wakati watu wengi walihisi kwamba Sasha na Malia hawakua na furaha kuwa na baba yao katika hafla ile na hata kulizungumzia swala hilo kwenye mitandao ya kijamii,Bi Lauten aliamua kujitoa kimasomaso na kuwakosoa wasichana hao kupitia kwa Facebook.
Sasha na Malia ni miongoni mwa vijana wadogo sana kuwahi kuwa katika ikulu ya White house
Mwanamke huyo akiomba msamaha, alisema baada ya kufanya maombi na hata kuzungumza na wazazi wake na kisha kusoma maandiko yake kuwahusu Sasha na Malia, alihisi kweli aliwakera wasichana hao.
"ningependa kuomba radhi kwa wote niliowaudhi kwa matamshi yangu, na nina ahidi kujifunza na kubadilisha mwenendo wangu, '' alisema Lauten.

No comments:

Post a Comment