Tuesday, December 2, 2014

Tuzo Fifa:Ronaldo,Messi,Neuer nani bora?



Lionel Messi
Shirikisho la Mpira wa miguu duniani Fifa limewataja Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na Manuel Neuer kuwania Tuzo ya mchezaji bora wa Dunia.Nyota hawa watatu wameteuliwa toka katika kundi la Wachezaji 23 waliokua wakiwania tuzo hii ya mchezaji bora itakayotolewa tarehe 12, Januari.
Nadine Kessler(Ujerumani) , Marta(Brazil) na Abby Wambach(Marekani) watawania tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa Wanawake.

Kwa upande wa Makocha watakaochuana katika kuwania Kocha bora wa mwaka ni pamoja na kocha wa mabigwa wa dunia Ujerumani Joachim Low,kocha wa Real Carlo Ancelotti,na Diego Simeone kocha wa Atletico Madrid.
Manuel Neuer
Kwa upande wa kocha bora wa kike ni pamoja na kocha wa Wolfsburg Ralf Kellermann,kocha wa timu ya Taifa ya Ujeruman chini ya miaka 20 Maren Meinert,na Norio Sasaki kocha wa Japan.
Cristiano Ronaldo 29, atakuwa akiwania tuzo hii kwa mara ya tatu mara baada ya kuitwaa mara mbili. Lionel Messi 27 akitaka kuweka historia ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mara ya tano.huku kipa Manuel Neuer akiwania tuzo hiyo kwa mara ya kwanza na iwapo atatwaa tuzo hii ataweka historia kuwa mchezaji bora golikipa toka ilipowekwa historia na kipa Lev Ivanovich Yashin mwaka 1963.
Nyota wengine waliokuepo katika kinyanganyiro hiki kabla ya kuenguliwa ni pamoja na Angel di Maria,Eden Hazard,Yaya Toure,James Rodrigues,Zlatan Ibrahimovic ,Gareth Bale na Neymer.

No comments:

Post a Comment