Tuesday, December 2, 2014

KIBARUA CHA RAIS UHURU KENYATTA


Kibarua kinachomkabili Rais Uhuru Kenyatta




Pichja ya kusikitisha ya mauaji ya walimu waliokuwa wanasafiri kutoka Mandera siku kumi zilizopita

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuhutubia taifa kwa mara nyingine baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kufanya shambulizi lengine la kinyama katika mji wa Mandera Kaskazini mwa Ke
nya.
Shambulizi lililolfanywa Jumanne asubuhi dhidi ya wafanyakazi wa mgodini mjini Madera Kaskazini mwa Kenya, limetokea siku kumi baada ya shambulizi lengine kama hilo dhidi ya basi lililokuwa limewabeba wasafriki wengi wakiwemo walimu kutoka Mandera.
Watu 28 waliuawa katika shambulizi la kwanza wiki jana.
Mji huu wa Mandera unapakana na Somalia na Ethiopia. Mandera ni mji wenye idadi kubwa ya wakenya wenye asili ya kisomali wengi ambao ni waisilamu.



Upinzani umekuwa ukitoa wito kwa serikali kufanyia mabadiliko idara ya usalama

Mashambulizi ya leo bila shaka yataathiri uchumi na mfumo wa kijamii wa eneo hilo, kwani wengi wa wafanyakazi walio mjini humo ni vibarua tu na vibaria wenyewe pia sio waisilamu na pia wanatoka katika maeneo mengine ya nchi.
Wengi wa wafnyakazi hao ni walimu na wauguzi na wachimba migodi lakini kwa sasa wameanza kuutoroka mji huo baada ya shambulizi la wiki jana.
Tetesi zinasema hali hii ya watu kutoroka na kurejea makwao huenda ikaendelea.
Punde baada ya mashambulizi ya wiki jana , mshauri wa Rais anayetoka Mandera, Abdikadir Mohamed alionya kuwa kundi la Al Shabaab linajaribu kuanzisha vita kwa msingi wa dini.



Rais Kenyatta mwenyewe ametakiwa ajiuzulu kwa kushindwa kubadili hali ya usalama nchini kwani mashambulizi yamekuwa mengi

Baadhi ya wakristo, pia wamewakosoa viongozi wa kiisilamu kwa kukosa kufanya juhudi za kutosha kukabiliana na kuenea kwa itikadi kali za kidini miongoni mwa waumini wa kiisilamu na hata miongoni mwa viongozi wenyewe.
Serikali ya Kenya nayo imelaumiwa kwa kukosa kuchukua hatua za kutosha kudhibiti usalama na shambulizi la hivi karibuni bila shaka litamuongeza shinikizo Rais Kenyatta za kukabiliana na mashambulizi hayo.
Upinzani umekuwa ukitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kujizulu hasa kwa kuwa ameshindwa kukabiliana na hali ya utovu wa usalama nchini humo. Hata hivyo Rais Kenyatta emekuwa akisisitiza kwamba kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha usalama unan

No comments:

Post a Comment