Mzee Yusuf akiwadatisha mashabiki kwa ngoma zake kali.
Mzee Yusuf akicharaza gitaa.
Diamond akimtambulisha kwa mashabiki mshindi wa zaidi ya milioni 500 za Big Brother Hotshots, Idris Sultan.
Idris
Sultan akimtambulisha kwa mashabiki wa Dar Live mshikaji wake aliyekuwa
naye kwenye mjengo wa BBA, Samantha wa Afrika Kusini.
Diamond akichana mistari ya wimbo wa Muziki Gani na mshikaji aliyepanda stejini kumwakilisha Nay wa Mitego.
NIMEMALIZA:
Diamond baada ya kuwakonga nyoyo mashabiki wake waliofurika Dar Live na
wao kuridhika aliamua kupozi nao kwa picha hii.
Diamond
akisalimia na msanii wa filamu, Yusuf Mlela baada ya kutangazwa kuwa
mshindi wa shindano la Ijumaa Sexiest Bachelor. Taji hilo alikuwa nalo
Mlela.
Diamond akipokea tuzo ya Ijumaa Sexiest Bachelor kutoka kwa Mkurugenzi wa Kijumosi Traders Ltd, Mohammed Mustapha.
Mhariri
wa Gazeti la Ijumaa waandaaji wa shindano hilo, Amran Kaima akimkabidhi
Ijumaa Sexiest Bachelor 2014/15, Diamond Platnumz cheti.
Mzee Yusuf akikandamiza kinanda wakati wa shoo yake Dar Live.
Mzee Yusuf na vijana wake wakifanya yao stejini.
Mzee Yusuf akionyesha ujuzi wa kucharaza gitaa chini kwa chini.
MFALME wa
Bongo Fleva, Nasibu Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa Krismasi
amewadhihirishia mashabiki wake kuwa ni mfalme baada ya kufanya makamuzi
ya hatari katika Ukumbi wa Dar Live, Mbagala-Zakhem, jijini Dar.Staa huyo aligonga ngoma zake zote na kuzikonga vilivyo nyoyo za mashabiki waliofurika katika uwanja huo wa burudani.
Mbali na Diamond, Mfalme wa Taarab nchini, Mzee Yusuf naye alifanya shoo kali na kuwapagawisha mashabiki waliofika kwa wingi kuliko siku zote katika ukumbi huo wa kisasa wa Dar Live.