MAMIA ya wakazi wa jijini Dar es Salaam jana walifurika katika ufukwe wa Coco Beach ili kupata burudani mbalimbali, hususani muziki, kusherehekea Sikukuu ya Krismasi ambapo Kampuni ya Vodacom ilifanya tamasha kubwa sehemu hiyo iliyovutia watu wa kila aina.