Saturday, June 21, 2014

Kijiji karibu na Chibok chashambuliwa

Ripoti zinasema kuwa shambulio jengine limetokea katika kijiji kimoja cha kaskazini-mashariki mwa Nigeria, karibu na pahala ambapo wasichana wa shule zaidi ya mia-mbili walitekwa nyara. Chibok, NigeriaKiongozi mmoja wa kijiji aliiambia BBC kwamba watu waliokuwa na silaha walivamia kijiji cha Koronginim, kama kilomita 14 kutoka Chibok ambako wasichana walitekwa na wapiganaji Waislamu wa kundi la Boko Haram mwezi Aprili.
Alieleza kuwa watu kama watatu waliuwawa na
kwamba kijiji hicho kimeteketezwa na moto.
Aliongeza kusema anafikiri washambuliaji walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.